Katika hali isiyokuwa ya kawaida Watu wanne wa familia moja wamenusurika kifo baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na mmoja wa wanafamilia hao ambaye alijimwagia mafuta ya Petroli nakisha kuwasha moto wakati huo akiwa amejifungia ndani ya nyumba hiyo.
Augustino Elius mmoja wa majeruhi hao amesema ndugu yao huyo aitwae Pascal Elius (mtuhumiwa) aliwaita ndani wakiwa watatu na mtuhumiwa wa nne Ili awaeleze changamoto zake za kiafya lakini galfa alichukua mafuta na kuwagia kisha kuwachoma na kuwachoma moto ambapo nyumba ilitekekea na moto na kusababisha wote wanne kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Alex Mkama, amesema tukio hilo la moto limetokea kijiji cha Gonja kata ya Pemba Wilaya ya Mvomero, ambapo kwasasa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo wakati majeruhi hao wakiendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro huku mtuhumiwa akiendelea kupatiwa matibabu chini ya ulinzi.
Muuguzi wa Zamu Hospitali ya Rufaa mkaoa Morogoro Devotha Msungus amesema majeruhi hao wamepata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao, wawili kati yao wamelazimika kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi na Wawili wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.