Watu 11 wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea katika kiwanda cha kuzalisha sukari Mtibwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema “Tukio limetokea Saa 7:30 Usiku kuamkia leo Mei 23, 2024, kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme. Waliofariki ni Wataalamu wa Umeme na Mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo” Amesema kati ya waliofariki kuna Raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil ambapo miili ya wote waliopoteza Maisha imehifadhiwa Hospitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala
Kulingana na Marugujo, mlipuko huo ulitokea wakati wafanyakazi wa kiwanda hicho wakijiandaa na uzalishaji wa bidhaa hiyo.
"Ni kweli kuwa tukio la namna hiyo limetokea ndani ya kiwanda cha Mtibwa, na ni jambo la kawaida kuwepo na joto la kiwango fulani ili sukari iweze kuzalishwa," ameeleza.
Marugujo ameongeza kuwa timu ya waataalamu imepiga kambi katika kiwanda hicho ili ili kuweza kubaini chanzo halisi cha kutokea kwa mlipuko huo.
vifo vyafikia 13 ajali mtibwa.