Maisha ya siasa
Mbunge huyo anasema kuwa alijiingiza
katika siasa kipindi cha Chama cha
Tanu mwaka 1976 wakati huo akiwa
mwanafunzi wa Sekondari, Forest na
kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tanu
tawi la shule na mwaka 1997 CCM
ilipozaliwa alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafuzi.
Anasema kuwa baada ya kuhitimu
masomo yake alijishughulisha na
biashara mpaka mwaka 1992 CCM
ilimteua nafasi ya mwekahazina nafsi
aliyodumu nayo mapaka mwaka 1990
baada ya kuteuliwa na Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro wakati huo, Yusufu
Makamba kuwa Mwenyekiti wa Kamati
ya saidia Moro ishinde na kupitia timu
ya Reli waliiwezesha kushinda na
kuhiriki mashindano mbalimbali.
"Kamati ile ilinipa umaarufu mkubwa
hivyo nikashauriwa kugombea nafasi ya
uwekahazina mkkoani Morogoro vijijini
nafasi niliyodumu nayo mpaka mwaka
1997.
Kwa mujibu wa Sadiq, mwaka 1997
aliamua kugombea ubunge Jimbo la
Morogoro Kaskazini baada ya aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo, Nikas Mahindakufariki dunia na kuwashinda
wagombea wengine saba.
"Nilidumu kwa miaka mitatu kwa kuwa
ulikuwa ni uchanguzi mdogo na mwaka
2000 ukafanyika Uchaguzi Mkuu
nikagombea na kushinda tena."
Ajivunia kuanzishwa kwa halmashauri
ya Mvomero
Kwa mujibu wa Sadiq, mwaka 2001
alikutana na Rais wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa pamoja na Waziri
Mkuu, Frederick Sumaye na
kuwasilisha ombi la jimbo hilo
ligawanywe na kupata wilaya jambo
lilifanikiwa ambapo mwaka 2005
ilianzishwa Halmashauri ya Wilaya ya
Mvomero na mwaka huo huo aligombea
tena jimbo hilo na kushinda.
Anyang'anywa jimbo na Makala
Mwaka 2010 Sadiq alipata upinzani
mkubwa kutoka kwa kada mwenzake,
Makala na kupoteza kiti hicho. Baada ya
uchaguzi huo Makala aliteuliwa kuwa
mmoja wa mawaziri katika Serikali ya
awamu ya nne.Kwa mujibu wa Sadiq, mizengwe na
fitna ndivyo vilivyomfanya apoteze
nafasi hiyo na kujikuta ikienda kwa
hasimu wake wa siasa.
Ashinda tena ubunge Mvomero
Kama kile kinachoonekana kuviziana na
mpinzani wake, Sadiq anajitosa tena
katika kinyang'anyiro cha kugombea
ubunge katika jimbo hilo na safari hii
anafanikiwa kumbwaga mpinzani wake
huyo.
Siri ya ushindi
Mbunge huyo ambaye pia alikuwa
akimiliki wa mabasi ya Sadiq line na
vituo vya mafuta mjini Morogoro
anasema, siri ya ushindi iliyosababisha
kurudi katika kiti hiko ni kutokata
tamaa, kuwa jasiri na kufanya vitu
ambavyo leo vina mhukumu.
“Mwaka 2008 tulikubaliana tuweke lami
kutoka Magole, Turiani kwenda Handeni
na Dumnila, Kilosa hadi Mikumina 2009
maandalizi yalianza lakini nilipotoka
madarakani mradi huo ulisimama,
wananchi wamepima na kugundua
kuwa walifanya makosa.
Changamoto
Sadiq anasema migogoro ya wakulima
na wafugaji ndiyo changamoto kubwa
jimboni kwake jambo analodai inabidi
kutumia busara ili kupatiwa ufumbuzi
pia kutokuwa na maji safi na salama
wakati uhaba wa ardhi ya kilimo na
pembejeo pamoja na umaskini wa
wananchi bado ni tatizo kubwa.
Sadiq anasema amejipanga kusimamia
kwa nguvu zake zote ilani ya chama
chake ili iweze kutekelezeka lakini pia
kutekeleza miradi yote aliyoianzisha
pamoja na iliyoanzishwa na mpinzani
wake.
"Nitashirikiana na wataalamu na
viongozi wa wilaya kuhakikisha ahadi
zote za Rais zinakamilika ikiwa ni
pamoja na kumuomba afute hati zote za
mashamba yaliyopewa wawekezaji
ambao wameshindwa kuyaendeleza ili
yarudishwe kwa wananchi kwaajili ya
kilimo kwani kwakufanya hivyo
tutaongeza pato la mwananchỉ mmoja
mmoja na hatimnaye kukuza uchumi."
Sadiq anawataka vijana kuwa
waaminifu na kutokata tamaa lakini
kikubwa ni kutangulize Mungu katika
mambo yao hukuakitoa mfano wa jinsi yeye alivyopata misukosuko katika
siasa, lakini alipambana hadi
akahakikisha anarudi katika jimbo hilo.
Anamudu vipi biashara, siasa na
familia?
“Namshukuru Mungu kwani familia
yangu inaniunga mkono hata nilipopata
misukosuko ya siasa haikunitupa jambo
linalosababisha nimudu vyema
shughuli zangu zote."
Mbunge huyo anasema anapenda
kuangalia mpira, kusafiri pamoja na
familia yake lakini pia kuhakikisha
anafanya biashara kwa nguvu zake zote.
Awapa somo vijana waendesha
bodaboda
"Vijana wanaojishughulisha na biashara
ya bodaboda wakiwezeshwa ni sehemu
ya ajira hivyo nimeamua kuunda
vikundi maalumu kwaajili ya
kuwasaidia pia wafanyabiashara
ndogondogo wakiwamo mamalishe na
nitahakikisha natumia mfuko wa jimbo
pamoja fedha zangu kuwaongezea
mitaji ili waweze kufanya biashara
yenye tija."
Anasema kwa sasa vipaumbele vyake ni
kilimo. ajira mitaji kwa makundi yote,Anasena kwa sasa vipaumbele vyake ni
kilimo, ajira mitaji
kuondoa kero kubwa ya elimu, maji,
afya kwa wazee ili wapate matibabu
bora na lakini pia Hospitali ya Turiani
inakuwa ya Teule.