Maafisa waandikishaji wa daftari la orodha ya wapiga kura kutoka Tarafa za Mvomero na Turiani tarehe 07 Oktob, 2024 wamepatiwa mafunzo ya uandikishaji wa wapiga kura ngazi ya Vijiji na Vitongoji zoezi hilo la kuandikisha linatarajiwa kuanza tarehe 11 - 20 Oktoba, 2024.
Akifungua mafunzo kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi, Mjumbe wa Sekretarieti ya uchaguzi Bi. Mary Kayowa amewataka washiriki kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo ya Serikali katika zoezi hili kufikia lengo la kuandikisha watu wote wenye sifa za kupiga kura.
Aidha amewataka kufika kwenye Vituo vya kuandisha wapiga kura kwa muda uliopangwa ambapo vituo vitafunguliwa saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni. Pia amesisitiza suala la kutovaa mavazi yenye mlengo wa chama chochote cha siasa. na kwamba hatarajii kusikia mtu ameharibu kwa uzembe badala yake zikamilike kama maelekezo yalivyotolewa na Serikali.
Naye, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndg. Gabriel Mollel amesisitiza umuhimu wa zoezi hilo kufanyika kwa umakini na uwazi ili kuhakikisha zoezi linafanikiwa.